Vuguvugu la Sunni lenye msimamo
mkali la ISIS ambalo limeteka maeneo ya Kaskazini mwa Iraq limesambaza
picha ambazo zinaonyesha jinsi wapiganaji wake walivyoangamiza idadi
kubwa ya wanajeshi wa Iraq.
Picha zinazosambazwa kupitia internet
zinaonyesha miili ya watu iliyosongamana ndani ya mtaro ikiwa imepelekwa
hapo kwa kutumia malori.Wapiganaji wa ISIS wanaonekana wakibeba bendera nyeusi ya huku wakichoma miili hiyo na kulazimisha mateka kulala chini.
ISIS yachapisha picha za mauaji ya majeshi ya Iraq .
Site yetu haijaweza kuthibitisha uhalali ya picha hizo kikamilifu lakini iwapo ni za kweli mauaji hayo yatakuwa mojawapo ya matukio mabaya zaidi kuwahi kuikumba Iraq tangu majeshi ya Marekani kuingia nchini humo mwaka 2003.
Duru kutoka vuguvugu la waasi zinasema idadi kubwa ya watu waliotekwa wameuawa.
Mji wa Tikrit ulitekwa na waasi Jumatano wiki iliyopita na majeshi ya Iraq yalikubali kushindwa bila pingamizi.
Tumehamia
katika site hii mpya na bado tuko katika maboresho,hii ni katika hatua za awali
kabisa kuiboresha site yetu na utoaji wa habari na burudani.Vitu vingi
vitaonekana katika site hii mpya hivi karibuni.Endelea kutembelea www.bantutz.com
0 comments:
Post a Comment