Sheria mpya za kazi zimeanzishwa nchini Saudi Arabia kwa watu wanaofanya kazi nje, kwenye jua.
Kutoka 
sasa hadi September, vibarua hawaruhusiwi kufanya kazi nje kutoka saa 6 
mchana hadi 9 jioni, kwa sababu ya masilahi ya afya yao.
Wafanyakazi
 kwenye mitambo ya mafuta na kazi za lazima za ukarabati, hawahusishwi 
na uamuzi huo ikiwa hatua zinachukuliwa kuwakinga na jua.
Nchi 
jirani ya Qatar, imelaumiwa sana kwa kuwalazimisha vibarua kutoka India 
kufanya kazi kutwa nje, wakijenga mwahala mwa mashindano ya kandanda ya 
mwaka wa 2022.
Imesema itachukua hatua kufanya mazingira yao ya kazi kuwa bora.
Tumehamia
katika site hii mpya na bado tuko katika maboresho,hii ni katika hatua za awali
kabisa kuiboresha site yetu na utoaji wa habari na burudani.Vitu vingi
vitaonekana katika site hii mpya hivi karibuni.Endelea kutembelea www.bantutz.com

0 comments:
Post a Comment