Facebook

Sunday, 1 June 2014

Madai ya ufisadi dhidi ya FIFA yatolewa

Katibu mkuu wa shirikisho la FIFA duniani Sepp Blatter

Madai mapya ya ufisadi yametolewa dhidi ya shirikisho la soka duniani FIFA kuhusiana na utata uliosababisha taifa la Qatar kupewa rukhsa ya kuandaa michuano ya kombe la dunia ya mwaka 2022.
Gazeti la Sunday Times kutoka Uingereza limesema kuwa limepata stakhabadhi zinazoonyesha vile aliyekuwa afisa wa shirikisho hilo nchini Qatar Mohammed bin Hammam alivyowalipa mamilioni ya madola maafisa wa soka kwa madhumuni ya kuiunga mkono Qatar kuandaa mechi hizo.
Bwana Hammam amekataa kujibu madai hayo mapya.
Lakini mwandishi anayesimamia michezo amesema kuwa wataishinikiza FIFA kuanzisha kura mpya ya kuandaa michuano hiyo ya mwaka 2022.

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment