Facebook

Tuesday, 10 June 2014

Man United kumuuza Fellaini kwa bei ya hasara


Nyota wa Ubelgiji na Manchester United Marouane Fellaini. Viongozi wa United wako tayari kumuuza kwa bei ya hasara.
Nyota wa Ubelgiji na Manchester United Marouane Fellaini. Viongozi wa United wako tayari kumuuza kwa bei ya hasara.
Katika jitihada kuisafisha sahani na kusahau kabisa nyayo za wakati wa David Moyes, viongozi wa Old Trafford wanataka kumfuta Fellaini kwenye vitabu – hata kwa hasara ya pauni milioni 15.
Mbelgiji huyo ambaye alisajiliwa kwa pauni milioni 27.5 na kucheza kipindi cha miezi ya David Moyes Old Trafford, atakuwa wa kwanza kutolewa mlangoni na Louis van Gaal.
Wanafikiria kuchukua hata pauni milioni 12 kwa mtu ambaye walimnunua kwa kiasi kinachokaribia pauni milioni 30 kwa muda ulipita usiopungua mwaka.
Fellaini angeweza kuwa mmoja wa wengi ambao Van Gaal angeweza kumuwekea matumaini kwenye klabu yake mpya.
Van Gaal amepewa kitita cha pauni milioni 200 ili kuimarisha kikosi chake, huku nyota wa Southampton Luke Shaw akitarajiwa kuwa wa kwanza kusaini msimu huu mpya.
Shaw aliiambia Saints kuwa anataka kuondoka klabuni Mei 11, siku ya mwisho ya msimu wa mwisho.


Tuko katika maboresho hivi karibuni blog hii itakuwa ni site ambayo itaitwa www.bantutz.com ni katika hatua za kuboresha huduma zetu za kutoa habari na burudani.Tutakuja katika muonekano mpya na bora zaidi.Vitu vizuri vipya usivyotarajia utaviona na kufurahia kupitia www.bantutz.com....

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment