Facebook

Tuesday, 17 June 2014

Michael Jordan ndiye mwanamichezo bilionea kwa sasa duniani.

Michael Jordan akiwa Chicago Bulls ambapo alikuwa bingwa mara sita akiwa na timu hiyo yenye maskani yaje Chicago, Ilinois.
Michael Jordan akiwa Chicago Bulls ambapo alikuwa bingwa mara sita akiwa na timu hiyo yenye maskani yake Chicago.
Gwiji wa mpira wa kikapu Michal Jordan amekuwa bilionea wa sasa ambaye amepata umaarufu wa ghafla kwa kuwa mwanamichezo mashuhuri.
Forbes wanakadiria kuwa Jordan yuko sawa na mmiliki wa Charlotte Hornets kwa dola milioni 416 huku utajiri wake nje ya timu ukiwa ni dola milioni 600.
Iliripotiwa kuwa Jordan anamiliki asilimia 89.5 ya Hornets, huku ikiashiria kuongezeka kwa hisa kwenye timu hiyo ambapo awali alimiliki asilimia 80.
Msemaji wa Jordan, Estee Portnoy, alithibitisha kwamba Jordan alinunua hisa za ziada kwenye timu ya Hornets mwezi Januari 2013, ila hakusema kiasi gani.
Portnoy hakutoa maoni kuwa Jordan ni bilionea au la.
Bingwa wa NBA mara sita akiwa na Chicago Bulls, Jordan alipata umaarufu na bahati kwenye mpira wa kikapu, vile vile na kuigiza filamu.
Nyota huyo, 51, alikuwa mmiliki mkubwa wa Hornets (iliyoitwa Bobcats zamani) mwaka 2010 wakati aliponunua hisa za dola milioni 175 kutoka kwa Bob Johnson.


Tumehamia katika site hii mpya na bado tuko katika maboresho,hii ni katika hatua za awali kabisa kuiboresha site yetu na utoaji wa habari na burudani.Vitu vingi vitaonekana katika site hii mpya hivi karibuni.Endelea kutembelea www.bantutz.com

0 comments:

Post a Comment