Ndege zisizo na rubani zitaanza
kutumiwa na Umoja wa Mataifa nchini Mali kukabiliana na utovu wa usalama
eneo la Kaskazini mwa nchi hiyo.
Mkuu wa kikosi cha usalama cha Umoja huo, aliambia baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuwa watasadia serikali kuwalinda raia.Waasi wa Tuareg bado wanaendesha harakati zao katika eneo la Kaskazini mwa nchi hiyo.
Waziri wa mambo ya nje wa Mali,Abdoulaye, alisema kuwa serikali ingependa huduma za ndege zisizo na rubani kuanza haraka iwezekanavyo.
Baada ya vita mjini Kidal mwezi Mei, makundi matatu ya waasi wa Tuareg yalikubaliana kusitisha vita.
Bwana Ladsous alisema kuwa ndege hizo, zitatumiwa kuimarisha usalama na kuhakikisha kuwa raia wa kawaida wanapata ulinzi wa kutosha.
Pia alisisitiza umuhimu wa mazungumzo ya amani na kudhibiti hali ya usalama ambayo inaendelea kudorora.
0 comments:
Post a Comment