Facebook

Friday, 20 June 2014

Wanaharakati 8 washtakiwa Mombasa, Kenya

Mombasa ni moja ya miji ambayo imeshuhudia utovu mkubwa wa usalama
Wanaharakati wanane wamefunguliwa mashitaka mjini Mombasa Pwani ya Kenya wakituhumiwa kwa kuhusika na maandamano haramu.
Awali wanaharakati hao walikamatwa wakati wa maandamano yao kupinga kile walichosema ni serikali kukosa na kushindwa kudhibiti usamala nchini Kenya.
Gari la mmoja wa wanaharakati hao pia lilikamatwa.
Miongoni mwa waliokamatwa ni pamoja na maafisa wa shirika la kitaifa la kutetea haki za binadamu tawi la Mombasa.
Wanaharakati hao walifikishwa mahakamani na kusihitakiwa ingawa baadaye waliachiliwa kwa dhamana.
Baadhi yao walivamia kituo cha polisi wakiwataka wenzao kuachiliwa
Wanaharakati hao wamekosoa polisi kwa kuzuia maandamano yao ambayo wanasema ni haki yao ya kikatiba.
Wanawalumu kwa kuyaingilia ili kuwatawanya wakitumia gesi ya kutoa machozi.
Kenya imekuwa ikikumbwa na hali mbaya ya usalama pakishuhudiwa mashambulizio ya kigaidi kama yaliyotokea Jumapili usiku ambapo watu zaidi ya sitini waliuawa.

0 comments:

Post a Comment