Facebook

Monday, 16 June 2014

Roy Hodgson: Ninaamini England itafuzu

Roy Hodgson

Kocha wa England, Roy Hodgson, ana imani kubwa na kikosi chake kufuzu raundi ya 16 bora ya Kombe la Dunia pamoja na kufungwa 2-1 na Italia mjini Manaus.
Daniel Sturridge alisawazisha goli la Claudio Marchisio wa Italia, ila Mario Balotelli aliwapa Azzuri ushindi.
“Hakuna mashaka kuwa tulicheza vizuri kama timu, hasa kipindi nikiwa nao,” alisema Hodgson.
“Ni ngumu kukubali kuwa tulipoteza. Ila nina imani kubwa kuwa tunafanya vizuri zaidi kwenye mechi zijazo na kufudhu.”
England watavaana na Uruguay siku ya Alhamisi kabla ya kumaliza mechi zao za Kundi D dhidi ya Costa Rica siku ya Jumanne, Juni 24.



Tumehamia katika site hii mpya na bado tuko katika maboresho,hii ni katika hatua za awali kabisa kuiboresha site yetu na utoaji wa habari na burudani.Vitu vingi vitaonekana katika site hii mpya hivi karibuni.Endelea kutembelea www.bantutz.com

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment