Facebook

Monday, 16 June 2014

Bajaj zazidi kuonekana katika maeneo ya Jiji la Dar

Bajaj ikiwa imebeba abiria katika eneo la Kivuko cha Feri jijini Dar es Salaam. Usafiri wa bajaj na bodaboda umekatazwa katika maeneo ya mji huo.
Bajaj ikiwa imebeba abiria katika eneo la Kivuko cha Feri jijini Dar es Salaam. Usafiri wa bajaj na bodaboda umekatazwa katika maeneo ya mji huo.

Baada ya bajaj na bodaboda kukatazwa kuonekana maeneo ya mji wa Dar Es Salaam, hali imekuwa tofauti kwa baadhi ya waendesha vyombo hivyo vya usafiri mjini.
Usafiri huo ambao umekuwa umaarufu mjini umeonekana kwenye kivuko cha Feri jijini Dar Es Salaam lakini ukiwa na waendeshaji tofauti, baadhi ya bajaj zilizoenekana maeneo hayo zilikuwa zinaendeshwa na baadhi wa walemavu.
Walemavu hao walionekana wakiendesha bajaj hizo huku wakiwa wamebeba abiria ambao ni ngumu kuruhusiwa kupanda kwenye daladala kutokana na mizigo yao, na hivyo kukimbilia usafiri huo.
Usafiri wa bajaj umekuwa maarufu katika jiji la Dar Es Salaam pamoja na kuzuiwa na serikali. Bajaj nyingine hutumiwa na walemavu kama njia yao ya kujipatia kipato, serikali inapaswa kuliangalia tena suala hilo.

Serikali
Labda serikali, inapaswa kulitazama agizo lao kwa jicho la umakini, kwani walemavu wamekuwa wakitumia bajaj hizo kama mkombozi kutafuta kitu cha kupeleka kinywani, hivyo kukataza usafiri mjini, kunapaswa kuzingatia watu wenye mahitaji muhimu kama hao walemavu.
Mwandishi wa Taarifa News aliekuwa eneo hilo amedai msururu wa bajaj hizo katika eneo hilo zikiwa zimepangwa kwa utaratibu mzuri huku zikiwabeba baadhi ya wananchi katika eneo hilo.
“Tena bajaj hizo zinaweza kufanyiwa marekebisho zikaendeshwa kwa urahisi na walemavu hawa, mfano, mlemavu wa miguu, anaweza kutumia bajaj ambayo itamfanya atumie mikono tu kuiendesha, serikali inapaswa kuliangalia hilo”, alieleza.

Tumehamia katika site hii mpya na bado tuko katika maboresho,hii ni katika hatua za awali kabisa kuiboresha site yetu na utoaji wa habari na burudani.Vitu vingi vitaonekana katika site hii mpya hivi karibuni.Endelea kutembelea www.bantutz.com

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment