Facebook

Sunday, 1 June 2014

Taifa Stars yataabika Zimbabwe

 Photo: TAIFA STARS WATAABIKA ZIMBWABWE
Gazeti la The Herard la nchini Zimbabwe limeandika kuwa wachezaji wa Taifa Stars Ijumaa hii walijikuta wakikaa nje baada ya uongozi wa hoteli hiyo, Pandhari Hotels kudai kutolipwa fedha na shirikiko la soka la Zimbabwe, ZIFA.
Wachezaji wa Taifa Stars walijiandikisha kwenye hoteli hiyo siku ya Alhamis na jana waliporejea kutoka kwenye mazoezi walikuta vyumba vyao vikiwa vimefungwa huku hoteli hiyo ikitaka ZIFA ilipe kwanza deni lao.
Shirikisho hilo linasemekana kudaiwa fedha nyingi na hoteli hiyo ambayo ilitumiwa pia na timu ya Taifa ya nchi hiyo siku zilizopita kuweka kambi yake. Waandishi wa The Herald walipofika kwenye hoteli hiyo waliwakuta wachezaji wa Taifa Stars wakiwa sehemu ya mapokezi na majonzi makubwa.
Kutokana na hali hiyo, balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe Adadi Rajabu naye alifika na kuelezea kusikitishwa kwake kutokana na hatua hiyo. Balozi huyo alidai kuwa hizo ni njama tu za kuwachanganya wachezaji wa Taifa Stars.
“Hatutarudishwa nyuma na njama hizi na tutacheza ili kushinda. Naamini wachezaji watasahau tukio hili na watajikita katika sababu iliyowaleta Zimbabwe,” balozi Rajabu aliliambia gazeti la Herard.
“Tunachoelewa ni kwamba hii ni njia ya makusudi ya kutuchanganya.”
Rajabu alikuwa akiongea na wachezaji wa stars kwenye eneo la kusubiria wageni katika hoteli hiyo. Hata hivyo baadaye usiku wa jana, suala hilo lilimalizika na wachezaji waliruhusiwa kuingia kwenye vyumba vyao katika hoteli hiyo.
Taifa Stars itacheza na Zimbabwe kesho. Katika mchezo wa kwanza uliofanyika jijini Dar es Salaam, Stars walishinda kwa bao moja.

Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com uweze kujua kila kitakachokuwa kinaendelea kuhusiana na mauza uza hayo yanayoendelea huko Zimbabwe
 
0 comments:

Post a Comment