Manchester United itasikiliza dau kwa timu inayotaka kumnunua kiungo wake Maroanne Fellaini, na wapo tayari kumuuza kwa pauni milioni 15, licha ya David Moyes kumnunua kwa pauni milioni 27 msimu uliopita (Times),
Rais wa Napoli Aurelio De
Laurentiis amepuuzia taarifa zinazomhusisha winga Lorenzo Insigne kwenda
Arsenal (Evening Standard),
Jose Mourinho amefutilia mbali nia ya Real
Madrid kumsajili Ramires (Daily Star),
Arsenal wanajipanga kumchukua
beki wa kulia wa Southampton, Callum Chambers, kuziba pengo la Bacary
Sagna (Daily Mirror),
Mshambuliaji wa Atlètico Madrid Diego Costa
amesema uhamisho wake wa pauni milioni 32 kwenda Chelsea uko karibu
kukamilika (Metro),
Hatua ya Manchester United kumsajili beki wa kushoto
wa Southampton, Luke Shaw iko mashakani baada ya Louis van Gaal kuanza
kumtazama Jordi Alba wa Barcelona (Daily Express),
QPR wanafikiria
kumfanya beki wa kati wa zamani wa Man U, Rio Ferdinand kuwa mchezaji
anayelipwa zaidi na klabu hiyo kwa kumpa pauni 80,000 kwa wiki
(Guardian),
Meneja wa Napoli Rafael Benitez anataka kumsajili Jermaine
Pennant, ambaye alikuwa naye Liverpool (Daily Mirror).
Share tetesi hizi
na wapenda soka wote. Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. !
Tuko katika maboresho hivi karibuni
blog hii itakuwa ni site ambayo itaitwa www.bantutz.com ni katika hatua za
kuboresha huduma zetu za kutoa habari na burudani.Tutakuja katika muonekano
mpya na bora zaidi.Vitu vizuri vipya usivyotarajia utaviona na kufurahia
kupitia www.bantutz.com....
0 comments:
Post a Comment