Arsenal huenda wakamkosa kipa wa Real Madrid, Iker Casillas, baada ya
mpenzi wake kudai kuwa hatohama kutoka mji mkuu wa Spain, Madrid (Daily
Express)
Lakini Arsenal huenda wakamsajili mshambuliaji wa Real Madrid
Alvaro Morata na wapo tayari kupambana
na Tottenham na Inter Milan wanaomtaka pia (Daily Express)
Barcelona
wamefikia makubaliano yasiyo rasmi na Marcus Reus wa Borussia Dortmund.
Reus amekuwa akifuatiliwa pia na Manchester United (Talksport)
Wakati
huohuo Manchester United wapo tayari kupokea pauni milioni 12 kwa kiungo
wake Marouanne Fellaini ambaye alisaini mwaka jana kutoka Everton kwa
pauni milioni 27 (Daily Star),
Chelsea wanajaribu kumsajili Cesc
Fabregas kutoka Barcelona katika mkataba ambao utahakikisha Arsenal
haipati nusu ya faida itakayopata Barcelona (Daily Telegraph),
Pepe
Reina atarejea Liverpool kwa kuwa Napoli inashindwa kufikia madai ya
Liverpool ya kubadili mkataba wa mkopo kuwa wa moja kwa moja (Metro),
Manchester City watakamilisha usajili wa beki wa kati kutoka Porto,
Fernando ifikapo mwisho wa wiki hii na pia kukamilisha usajili wa Bacary
Sagna kutoka Arsenal(Daily Mail),
Everton wana tumaini watafanikiwa
kupambana na Arsenal katika kumsajili Samuel Eto'o kutoka Chelsea (Daily
Express).
Share tetesi hizi na wapenzi wa soka. Tetesi nyingine kesho
tukijaaliwa.
Tuko katika maboresho hivi karibuni
blog hii itakuwa ni site ambayo itaitwa www.bantutz.com ni katika hatua za
kuboresha huduma zetu za kutoa habari na burudani.Tutakuja katika muonekano
mpya na bora zaidi.Vitu vizuri vipya usivyotarajia utaviona na kufurahia
kupitia www.bantutz.com....
0 comments:
Post a Comment