Liverpool, Arsenal na Manchester United
zinakabiliwa na ushindani kutoka Paris St- Germain kumsajili winga wa
Real Sociedad Antoine Griezmann.
Sociedad wanakata kumuuza mchezaji huyo kabla Kombe la Dunia halijaanza
(Daily Star),
Mshambuliaji wa QPR Loic Remy anataka kujiunga zaidi na
Arsenal kuliko timu yoyote (Daily Mirror),
Sunderland wametoa dau kutaka
kumsajili beki wa Swansea Ashley Williams (Sky Sports),
Chelsea wana
uhakika wa kumsajili Cesc Fabregas kutoka Barcelona kwa chini ya pauni
milioni 30 lakini watarekebisha mshahara wake wa pauni laki moja kwa
wiki (Times),
Winga wa Blackpool, Tom Ince ataamua kwenda Tottenham,
Everton au Newcastle, baada ya kukataa kwenda Inter Milan (Daily
Express),
Aston Villa wamemchombeza beki wa zamani Wa Man Utd Rio
Ferdinand, ingawa Rio mwenyewe anataka kuchezea timu ya London (Daily
Mail),
Liverpool wanakaribia kukamilisha usajili wa winga wa Bayern
Munich Xherdan Shaqiri (Daily Star),
Wakala wa Lorenzo Insigne anadai ni
heshima kubwa kuhusishwa na Arsenal, ambao wanajiandaa kutoa pauni
milioni 17 (Guardian),
Marseille wameanza mazungumzo na Newcastle kuhusu
kumsajili beki wa kati Mapou Yanga-Mbiwa (Newcastle Chronicle),
kiungo
wa Man City Samir Nasri huenda akasaini mkataba mpya wa miaka mitano
(Guardian),
Mshambuliaji wa Chelsea na Ubelgiji, Romelu Lukaku ameiambia
Chelsea kuwa anataka kuondoka Darajani ( Daily Telegraph).
Share tetesi
hizi na wapenda soka wote. Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa.
Tuko katika maboresho hivi karibuni
blog hii itakuwa ni site ambayo itaitwa www.bantutz.com ni katika hatua za
kuboresha huduma zetu za kutoa habari na burudani.Tutakuja katika muonekano
mpya na bora zaidi.Vitu vizuri vipya usivyotarajia utaviona na kufurahia
kupitia www.bantutz.com....
0 comments:
Post a Comment