Polisi wa Macau wanasema
wamegundua magengi mawili ya kamari ambayo yamepokea mamilioni ya dola
katika kamari ya kubahatisha matokeo ya mechi za Kombe la Dunia.
Maafisa wa polisi wamewakamata watu zaidi ya 20 kwenye hoteli katika mji huo wa kamari.Watu hao wamekuwa wakipokea simu kutoka sehemu mbalimbali za dunia, na mcheza kamari mmoja ametia dau la dola milioni-5.
Mwandishi mmoja mjini Hong Kong, jirani na Macau, anasema magengi hayo yakipata dola mia-moja-milioni kila siku kwa wateja wanaobahatisha matokeo ya Kombe la Dunia, na wateja wakiwasiliana nao kwa simu na kwenye internet.
Kati ya watu waliokamatwa 9 ni kutoka Malaysia, 4 kutoka Hong Kong na 13 kutoka Uchina bara
0 comments:
Post a Comment