Facebook

Saturday, 21 June 2014

Yaya na Kolo Toure wafiwa na mdogo wao, Ibrahim

Nyota wa Ivory Coast ndugu  Yaya Toure na Kolo Toure. Ndugu yao Ibrahim Toure amefariki wao wakiwa Brazil kwenye mashindano ya kombe la Dunia.

Nyota wa Ivory Coast Yaya na Kolo Toure wametaarifiwa kuhusu kifo cha mdogo wao wakati wakiwa kwenye Kombe la Dunia nchini Brazil.
Ibrahim Toure alifariki siku ya Alhamisi mjini Manchester, akiwa na umri wa miaka 28.
Chama cha Mpira wa miguu cha Ivory Coast kilisema: “Ujumbe wote wa Ivory Coast wanataka kuonyesha faraja na rambi rambi kwa wachezaji hao.
“Katika hali hiyo ya huzuni, timu nzima ya Ivory Coast na ujumbe mzima hapa Brazil, wanaungana mkono na ndugu wa Toure na familia kwa ujumla.”
Waliongeza: “Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu la Ivory Coast na Kamati Kuu wameomba Waivoriani kuwaombea dua”.
Ibrahim Toure alicheza kama mshambuliaji katika kipindi chote cha soka, hususani akiwa na timu ya Lebanon ya Al-Safa SC.
Poleni, endeleeni kulipigania taifa, Waivoriani wako nyuma yenu.

0 comments:

Post a Comment