Kelly Rowland alituma picha hii ikimuonyesha akiwa na ujauzito wa mtoto wake wa kwanza kwenye mtandao wa Instagram.
Mwanamuziki huyo, 33, aliolewa na meneja wake, Tim Witherspoon, mwezi uliopita kuliibuka tetesi zilizosambaaa haraka baada ya kutuma picha za harusi kwenye mtandao wa Instagram.
Ni mwaka uliopita tu, Kelly alikuwa mwenye furaja alipodai kuwa hakutaka kuanza kuwa na familia, akisisitiza kuwa anataka muda wa kuwa peke yake kabla ya kuanzisha familia.
Alisema: “Siko tayari, siko tayari kuwa na mtoto, hapana. Huo ndio ukweli. Kwa sababu kwa sasa, mi mbinafsi kidogo, sana – ningesema kidogo kidogo – ila bado ni mbinafsi.”
“Napenda muda wangu, nataka niamke muda ninaotaka, na nataka nitoke na kurudi ninavyopenda, hivyo sidhani kama nahitaji kutumia muda huo na mtu mwingine, sitaki kuharibu.”
0 comments:
Post a Comment