Facebook

Saturday 17 May 2014

Chuo cha Biashara CBE chamtimua Mhadhiri wake kwa Skendo za kula Uroda na Wanafunzi.



Chuo cha Biashara CBE chamtimua Mhadhiri wake kwa Skendo za kula Uroda na Wanafunzi.


Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), tawi la Dar es Salaam, kimemfukuza kazi mhadhiri wa chuo hicho anayedaiwa kuhusika na vitendo vya ukiukaji wa maadili ikiwamo kufanya ngono.
Mhadhiri huyo ambaye jina halikutajwa alinaswa na kamera za kisasa za kurekodi matukio za CCTV zilizofungwa kwenye vyumba vya madarasa ili kudhibiti nidhamu, miongoni mwa wanafunzi na wahadhiri.
Kamera hizo zimefungwa kwenye vyumba vya madarasa 20 ili kudhibiti vitendo vya ngono baina ya walimu na wanafunzi, wizi wa mitihani na matendo mengine yanayovunja sheria.
Hayo yalibainishwa jana jijini na mkuu wa chuo hicho, Profesa Emanuel Mjema, alipokuwa akizungumza na wanahabari wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Janeth Mbene.
Profesa Mjema, alisema, walifikia maamuzi ya kuweka kamera hizo za kisasa ndani ya madarasa Aprili mwaka jana baada ya kujiridhisha na taarifa za kuwapo matukio ya ukosefu wa maadili miongoni mwa wahadhiri ikiwa ni pamoja na kutoa alama za juu kwa baadhi ya wanafunzi wa kike baada ya vitendo vya ngono.

Endelea kutembelea katemimethsela,blogspot.com uweze kujua kila kitakachokuwa kinaendelea vyuoni..

0 comments:

Post a Comment