MAKUBWA! Kaburi la aliyekuwa Mnajimu Mashuhuri Afrika Mashariki, marehemu Shehe Yahya Hussein limejengwa tena baada ya hivi karibuni kubomolewa na watu wasiojulikana, lakini sasa limedaiwa kujengwa Kikristo na chini ya kiwango!
Akizungumza na Risasi Jumamosi juzi jijini Dar, msemaji wa familia ya Shehe Yahya, Maalim Hassan Yahya Hussein alisema kaburi hilo lipo kwenye Makaburi ya Tambaza karibu na Hospitali ya Muhimbili, Dar sanjari na lile la marehemu Shehe Kasim Bin Jumaa.
Alisema makaburi yote yalibomolewa wakati wa Operesheni Safisha Jiji ambapo serikali kupitia kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadik alikataa jiji kuhusika.
Hata Maalim Hassan alikiri si serikali iliyoyabomoa makaburi hayo bali ni wahuni wachache, lakini akasema mkuu wa mkoa aliahidi kwamba serikali itayajenga upya tena kwa kuyaboresha.
Familia hiyo ikasema inashangazwa makaburi hayo kujengwa katika mfumo wa makaburi ya Kikristo jambo ambalo halitoi picha nzuri kwa sababu wako watu wanatoka nje ya nchi kuja Tanzania kutaka kuliona kaburi la Shehe Yahya.
FAMILIA KUBOMOA
“Makaburi yale yalitakiwa kujengwa kwa kutumia kokoto maalum ziitwazo ‘mable’ na kulikuwa hakuna sababu ya kujenga ngazi ambazo watu wanaweza kukaa kama kaburi la marehemu Steven Kanumba.
“Kama marehemu alipokuwa hai hakukaliwa kwa nini akiwa amekufa akakaliwe akiwa ndani ya kaburi? Kule ni kumkosea heshima.
“Sisi kama familia tumeamua kwamba, lazima tuyabomoe makaburi yote, la baba na lile la marehemu Shehe Kassim siku ya Jumamosi (leo) na kuyajenga upya tutakavyo sisi tena kwa gharama zetu, serikali ibomoe matofali yao,” alisema Maalim Hassan
Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com uweze kufuatilia kila kitakachokuwa kinaendelea kuhusiana na sakata hili
0 comments:
Post a Comment