Monday, 19 May 2014
Kashfa nzito Bajeti ya Nishati na Madini
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na Mbunge wa Musoma Vijijini, Nimrod Mkono wameingia katika mvutano baada ya ujumbe wa maandishi wa kutaka kukwamisha bajeti ya wizara hiyo kusambazwa kwa wabunge.
Habari za uhakika zilizopatikana jana zilieleza kuwa kiini cha mgogoro huo ni ujumbe mfupi (SMS) ambao unamtuhumu Mkono kula njama za kutaka kukwamisha bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini.
Chanzo hicho limedokezwa kuwa, SMS hiyo inadaiwa kutumwa na Waziri Muhongo kwenda kwa baadhi ya wabunge akimtuhumu Mkono kuwahonga baadhi ya wabunge Sh3 milioni kila mmoja ili kukwamisha bajeti hiyo.
Ujumbe huo unasomeka ”Mhe Spika wa Bunge la Jamhuri, Sisi wabunge waadilifu tunakiri kwamba Mhe Mkono ametufuata na kutupatia fedha kila mmoja milioni 3 ili tukwamishe bajeti ya Nishati na Madini.
Ujumbe huo umeanza pia kusambaa kwenye mitandao ya kijamii ikiwamo Jamii Forums .
Mkono
Mkono ambaye pia ni Mwanasheria mashuhuri nchini, alipoulizwa jana kama ni kweli amelalamika kwa Spika juu ya jambo hilo, alikiri na kusema alichofanya ni kulalamika kwa Spika na amemwachia alishughulikie.
“Ni kweli nimelalamika kwa Spika. Unajua taratibu za Bunge ni kuna any complaint (lalamiko) unaliwasilisha officially (rasmi) kwa Spika… hilo jambo lipo nimelifikisha kwa Spika wao ndiyo watafuatilia kwa taratibu zao,”alisema.
Profesa Muhongo
Alipotafutwa kwa njia ya simu ili alitolee ufafanuzi suala hilo, Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo alituma ujumbe kwa simu ukisema:
“Tutavuka tukiwa na ushindi wa maskini na wanyonge wa nchini mwetu. Tutaendelea kujenga uchumi imara utakaotoa ajira mpya na matumaini mapya kwa vijana, maskini na wanyonge wa nchini mwetu. Watanzania wamechoshwa na wizi, udalali, ubabaishaji na rushwa.”
Mkurugenzi wa shughuli za Bunge, John Joel alipotafutwa jana alisema yeye hana taarifa juu ya jambo hilo akisema kama lipo, basi huenda likawa mikononi mwa Spika mwenyewe
Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com uweze kujua kitakachojiri kuhusiana na kashfa hii ndani ya Wizara ya Nishati na Madini
Related Posts:
Hussein Bashe amtetea Membe kuhusu Escrow.Duh hii sasa kali,nadhani kuna Mpango maaluum wa kupotosha Jambo la ESCROW na matumizi Mabaya ya Technology haya, Ingawa simuungi Mkono MEMBE katika NDOTO yake let's not make politics katika wizi huu mkubwa wa Nchii hii,Katik… Read More
Boko Haram lauwa watu 100 Nigeria.Ripoti kutoka kaskazini-mashariki mwa Nigeria zinaarifu kuwa kundi la wapiganaji Waislamu la Boko Haram, limefanya mashambulio mawili makubwa katika siku chache za karibuni ambapo watu karibu 100 wameuwawa. Kiongozi mmoja kat… Read More
BantuTz MAGAZINE-Soma kilichoandikwa katika Magazeti ya leo Novemba 24 BantuTz MAGAZETINI-Ni uratatibu ambao BantuTz imeuanzisha ili kuwawezesha wadau wote wa Bantu waweze kusoma na kupitia kurasa za magazeti mbalimbali nchini kila siku asubuhi ili kuwasogezea karibu zaidi huduma ku… Read More
BantuTz MAGAZETINI:SOMA KILICHOANDIKWA KATIKA KURASA ZA MBELE MAGAZETI YA LEO 23 Novemba. BantuTz MAGAZETINI-Ni uratatibu ambao BantuTz imeuanzisha ili kuwawezesha wadau wote wa Bantu waweze kusoma na kupitia kurasa za magazeti mbalimbali nchini kila siku asubuhi ili kuwasogezea karibu zaidi huduma… Read More
Mama Anne Kilango Malecela azushiwa ugonjwa wakati ni Ni Mzima Wa Afya Kumekuwa na uvumi unaosambazwa na genge la wahuni katika siasa kwamba mbunge wa jimbo la Same Mashariki ndugu Anne Kilango Malecela kuwa anaumwa sana.Wanaozusha maneno haya wanaenda mbali zaidi na kusema afya yake ime… Read More
0 comments:
Post a Comment