Facebook

Monday, 19 May 2014

Cristiano Ronaldo awafunika Messi na Diego Costa – atwaa tuzo ya PICHICHI


10314573_10150588744134953_7445809377026890214_nMshambuliaji wa klabu ya Real Madrid Cristiano Ronaldo amekuwa mfungaji bora na kutwaa tuzo ya PICHICHI ambayo hutolewa kwa mwanasoka anayekuwa kafunga magoli kwenye msimu mmoja wa La liga.
Ronaldo amemaliza msimu akiwa na magoli 30 baada ya kucheza 31 na kufanikiwa kuwazidi Diego Costa na Lionel Messi waliokuwa wakimfuatia kwa karibu. Pia Ronaldo amefungana kwa magoli na Luis Suarez katika kugombea tuzo ya kiatu cha dhahabu kinachotolewa kwa mfungaji bora wa ligi za ulaya.
Cristiano Ronaldo pia ni mfungaji bora wa michuano ya UEFA Champions League ambapo mpaka sasa ana magoli 16 huku bado akisubiri kucheza fainali dhidi ya Atletico Jumamosi ijayo.

0 comments:

Post a Comment