Facebook

Saturday, 17 May 2014

Paundi million 70 kumng'oa Luis Suarez Liverpool

Florentino perez.jpg
 
Real Madrid wametenga paundi milion 70 ili kumnasa straika wa Liverpool na mfungaji bora wa Ligu kuu England msimu huu Luis Suarez.
Real Madrid pia wanajipanga kumwachia Karim Benzema anayewaniwa na Arsenal na Man United.
Benzema amekua kivutio kikubwa kwa kocha Arsene Wenger na safari hii kuna uwezekano mkubwa akampata mkali huyo ili kuungana na Mesuit Ozil pale Emirates.
Taarifa zinasema kocha Wa Madrid Carlo Ancellot anavutiwa zaidi na Suarez wakati Rais wa klabu hiyo Florentino Perez yeye anavutiwa na Sergio Kun Aguero wa Man City na kuna kila dalili mmoja wa wakali hao akatua Santiago Bernabeu msimu ujao.
Liverpool wanaamini watambakiza Mshambuliaji huyo ambaye nusura ajiunge na Arsenal msimu ulioisha na pia wako katika harakati za kumsajili Anoine Griezmann toka Real Sociedad ili kujiimarisha zaidi baada ya kurudi katika ligi ya Mabingwa Ulaya.

UNADHANI SUAREZ ATAHAMA LIVERPOOL MSIMU UJAO?

0 comments:

Post a Comment