Facebook

Sunday, 15 June 2014

Capt.Komba amsifia mkewe baada ya kashfa nzito.

Sijawahi  kuona  mwanamke  mzuri  na  mwenye  imani  kama  mama  Komba ( Salome ) jamani, unajua  kulea  watoto  ambao  mama  zao  wapo  duniani  ni  kazi  sana,” alisema  Komba  katika  kipindi  cha  mkasi  kinachorushwa  na  East  African  Television

Mheshimiwa  Komba  alisema  ana  watoto  tisa  wakiwemo  wa  ndani  ya  ndoa  na  nje ya  ndoa  na  wote  wamelelewa  na  mke  wake  Salome  na  ndio  maana  anampenda  na  kumjali  kila  siku  za  maisha  yake  kwani  anastahili  kuitwa  mwanamke  haswa…..


John Komba  aliyasema  hayo  siku  chache  baada  ya  kuonekana  picha  zake  mbaya  za  kimahaba  alizopiga  akiwa  na  msichana  anayedaiwa  kuwa  ni  mpenzi  wake…..


Katika  mahojiano  na  kipindi  cha  Mkasi, John Komba  aliongelea  mambo  mengi  na  kusema  kuwa  ukiwa  kiongozi  na  mtu  mkubwa  nchini  ni  lazima  uzushiwe  mambo  yakiwamo  maradhi  makubwa  na  kashfa  mbalimbali…..


Sioni  ajabu  kuzushiwa  mambo  ambayo  sijayafanya  kwani  wanamuziki, wanasiasa  na  hata  viongozi  mbalimbali  wanakutana  na  mambo  ya  kuzushiwa  kwa  kuwa  wanajua  wakifanya  hivyo  watawaangusha  kutokana  na  vyeo  vyao  lakini  bado  tupo  bana,” alisema  Komba  huku  akicheka.

Komba  aliendelea  kuzungumza  kuwa  mwaka  2015  utakuwa  mwisho  wake  kuimba  na  anakusudia  kuwarithisha  vijana  wapya….

Mheshimiwa  Komba    alihitimisha  kwa  kusema  kuwa  katika  maisha  yake  hafikirii  suala  la  kufa  kwani  kifo  kipo  tu  hata  ukifikiria  na  kukaa  kuwaza  jambo  hilo  ni  kujitafutia  mkosi  tu  katika  maisha  yako. 




Tumehamia katika site hii mpya na bado tuko katika maboresho,hii ni katika hatua za awali kabisa kuiboresha site yetu na utoaji wa habari na burudani.Vitu vingi vitaonekana katika site hii mpya hivi karibuni.Endelea kutembelea www.bantutz.com

Related Posts:

  • Diamond aweka historia New Jersey  All Star Club Elizabeth New Jersey Diamond akikamua licha ya show kuchelewa kuanza na wapenzi wa Diamond kushikwa na jazba wakitaka aendelee lakini ikashindika kutokana na muda wa kufunga club kufika. &n… Read More
  • RAY C alitamani Penzi la kikongwe MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Rehema Chalamila ‘Ray C’, amesema kwa sasa hana mpango wa kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mtu, na kama ikitokea basi atamtaka kuwa na miaka kuanzia 60. Akizungumza katika… Read More
  • Mwimbaji wa Marekani Ray J matatani.... Mwimbaji wa Marekani Ray J amekamatwa na polisi mjini Beverly Hills kwa tuhuma za kuzozana katika baa ya hoteli ya Beverly Wilshire. Polisi wa Beverly Hills waliitwa baada ya kutokea malalamiko kuwa msanii huyo alimshi… Read More
  • Wasanii mbali mbali walipokuwa hospitalini wakisubiri mwili wa marehemu George Tyson Mwenyekiti wa Bongo Muvi, Steve Nyerere, akiwasili katika Hospitali ya Kairuki kusubiri mwili wa marehemu. Steve alivalia tisheti yenye ujumbe 'Why always me' Mke wa marehemu Tyson, Beatrice Shayo akiwa… Read More
  • Mtoto wa Pele jela miaka 33 Edinhio Pele alikuwa mlinda lango kabla ya kusataafu soka Mwanawe gwiji wa soka Brazil na duniani kote, Pele, Edinho Pele, amefungwa jela miaka 33 kwa kufanya biashara haramu ya pesa au kujipatia pesa chafu zilizoto… Read More

0 comments:

Post a Comment