LEJENDARI
wa Argentina, Diego Armando Marando, amewaponda Mabingwa wa Dunia Spain
kwa kushindwa kusoma alama za nyakati na sasa ‘tiki-taka’ imekufa baada
kufumuliwa Bao 5-1 na Netherlands Juzi kwenye Mechi ya Kundi B la
Fainali za Kombe la Dunia huko Brazil.
Vile vile, Maradona amemlaumu Kipa wa
Spain Iker Casillas kwa kufungisha Bao 2 na kusema hilo linaonyesha Jose
Mourinho hakufanya makosa alipomtema Kipa hiyo wakati akiwa Meneja wa
Real Madrid.
Juzi, Spain walibomolewa Bao 5-1 na
Netherlands licha ya wao kutangulia mbele kwa Bao 1 la Penati ya Xabi
Alonso lakini Netherlands wakaja juu na kushindilia Bao 5 kupitia Arjen
Robben na Robin van Persie, waliofunga Bao 2 kila mmoja, na Stefan De
Vrij kufunga 1.
Maradona anaamini Kikosi cha Kocha
Vicente del Bosque kimeshindwa kuchukulia kwa uzito onyo kutoka
Barcelona ambao Msimu huu walizorota mno na kutoka kapa bila Taji kubwa
lolote.
Maradona, mwenye Miaka 53, amenena:
“Timu ya Spain imezidi kuzeeka na hilo lilidhihirika walipocheza na
Netherlands. Spain wamekuwa wakicheza tiki-taka kwa muda sasa. Ni njia
njema kucheza Soka na Dunia nzima imefurahia. Iliwafanya washinde Mataji
matatu makubwa mfululizo kuanzia 2008 hadi 2012. Lakini Vicente del
Bosque angekumbuka Klabu huko Ulaya zishapata jibu la staili ya Barca
ambayo ni hiyo hiyo wanayocheza Timu ya Taifa ya Spain. Mchezo wa haraka
wa mashambulizi ya kaunta-ataki yamewazidi maarifa sasa! Lakini Spain
imegoma kubadilika licha ya wapinzani kugundua dawa yake! ”
Kipigo hicho cha Spain cha 5-1 ndicho
kikubwa kwa Bingwa Mtetezi wa Kombe la Dunia katika Mechi ya Kwanza na
hicho kilikuwa kipigo chao cha pili katika Mechi zao 55.
Maradona aliwasifia mno Robin van Persie na Arjen Robben na kumlaumu Kipa Iker Casillas kwamba hakucheza vizuri.
MARADONA: ‘MOURINHO NI SAHIHI KUHUSU CASILLAS!!’
Diego Maradona amesema uchezaji mbovu wa
Kipa Iker Casillas umedhihirisha Jose Mourinho hakukosea kumtema wakati
alipokuwa Meneja wa Real Madrid.
Mwenyewe Casillas amekubali kwamba
anapaswa kulaumiwa kwa kipigo hiki toka kwa Netherlands na Maradona
ameeleza: “Alikuwa na Gemu mbovu ambayo sijaona maishani..inanikumbusha
nini Rafiki yangu Mourinho alikuwa akiwaeleza Watu!”
Aliongeza: “Alisema Casillas hakuwa Kipa sahihi lakini badala yake hilo lilimfanya aondolewe Real!”
Tumehamia
katika site hii mpya na bado tuko katika maboresho,hii ni katika hatua za awali
kabisa kuiboresha site yetu na utoaji wa habari na burudani.Vitu vingi
vitaonekana katika site hii mpya hivi karibuni.Endelea kutembelea www.bantutz.com
0 comments:
Post a Comment