
Diego Costa amesema kwamba anajiunga na Chelsea kwa sababu 'ni moja ya klabu kubwa kabisa duniani'.
Straika huyo wa Atletico Madrid kwa muda mrefu sasa amekua akitarajiwa kumfuata Jose Mourinho katika dili linalofikia £32million na mchezaji huyo mwenye miaka 25 ametanabaisha kwamba dili hilo lipo karibuni kukamilika.
'Kwa nini nimechagua kuchezea Chelsea? Ni kwa sababu ni jambo linalokaribia kutokea,' Costa alisema
'Nimekua nataka kucheza Premier League kwa muda sasa. Chelsea ni moja kati ya klabu kubwa sana duniani kwa hiyo kuna vitu vingi hukufanya uchukue uamuzi kama huu.'
Costa atakua m-Spain wa pili kujiunga na Chelsea baada ya Fabregas kukamilisha usajili wa kutua Stamford Bridge wiki iliyopita
Tumehamia
katika site hii mpya na bado tuko katika maboresho,hii ni katika hatua za awali
kabisa kuiboresha site yetu na utoaji wa habari na burudani.Vitu vingi
vitaonekana katika site hii mpya hivi karibuni.Endelea kutembelea www.bantutz.com
0 comments:
Post a Comment