Facebook

Tuesday, 17 June 2014

Jeshi la Pakistan lawaandama Taliban

Wanajeshi wa Pakistan huko Waziristan Kaskazini
Mzozo wa mpakani kati ya Pakistan na Afghanistan ungali kutulia
Jeshi la Pakistan limeanzisha kile wanachoita operesheni kamili dhidi ya wapiganaji katika eneo la Waziristan Kaskazini, karibu na mpaka wa Afghanistan.
Katika taarifa iliyotolewa, jeshi lilieleza kuwa wanajeshi wamepewa kazi ya kuwafyeka magaidi ambao wamekuwa wakitumia ardhi ya Waziristan Kaskazini kama kambi yao, na kusababisha watu wengi kupoteza maisha yao na kuleta mtafaruku nchini.
Hapo awali, wakuu walisema kuwa wamemuuwa mtu anayeshukiwa kupanga mashambulio yaliyofanywa usiku mzima dhidi ya uwanja wa ndege wa Karachi juma lilopita.
Walisema kuwa, Abu Abdul Rehman al Maani, mwenye asili ya Uzbekistan, alikuwa mmoja kati ya wapiganaji 80 kutoka ndani na nje ya Pakistan, ambao waliuwawa katika mashambulio ya ndege yaliyofanywa Jumapili alfajiri Waziristan Kaskazini.


Tumehamia katika site hii mpya na bado tuko katika maboresho,hii ni katika hatua za awali kabisa kuiboresha site yetu na utoaji wa habari na burudani.Vitu vingi vitaonekana katika site hii mpya hivi karibuni.Endelea kutembelea www.bantutz.com

0 comments:

Post a Comment