Katika kuelekea komba la dunia 2014 nchini Brazil, Jeshi la Brazil limejipanga dhidi kwa vita dhidi ya dawa za kulevya zinazosambazwa mitaani na wauzaji wa dawa hizo maarufu kama mapusha.
Wafanya biashara hii haramu wameanza kujipanga kwa kutengeneza na kufunga dawa za kulevya kwa viwango vidogo dogo ili iwe raisi kubeba, kuuza na kusambaza.
Brazil inategemea wageni wengi na mashabiki wa soka kutoka nchi tofauti. Wageni zaidi ya laki sita watakuja Brazil kwa ajili wa kombe la dunia, Wageni/mashabiki wa soka elfu 10 kutoka Uingereza.
Biashara hii ya dawa za kulevya aina ya Cocaine italenga wageni na maeneo watakayofikia nchini Brazil.
Doria ya nguvu inafanywa na wanajeshi wa Brazil, zaidi ya vikosi elfu 30 vimemwagwa mitaani kwenye sehemu tofauti za nchi hio ilikukabiliana na uingizwaji wa dawa za kulevya kwaajili ya kombe la dunia.
Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com uweze kupata habari mbalimbali zitakazokuwa zinahusiana na michuano ya kombe la dunia
0 comments:
Post a Comment