Kwanza tutoe pole Kwa watu wote mliofikwa na maafa mbalimbali pamoja na
pole kwa kiongozi na mbunge wa Kigoma Zitto Kabwe kwa kufiwa na Mama
Yake mzazi.
Ni wiki sasa pamekuwa na gumzo hapa jijini juu ya tuhuma Za Ubakaji
zinazomkabili mume wa mwimbaji mashuhuri Flora Mbasha. Na Kwa Makusudi
na yamkini kikundi flani cha watu wamehusisha sakata hili na Kanisa letu
la Ufufuo na Uzima, tena Kwa maneno makali sana. Bahati mbaya watu hawa
wamewakosesha baadhi ya watanzania wasiojua Chochote na kujikuta nao
pia wamo kwenye kumbo la kutukana, kumkashifu na wakati mwingine
kutukana viongozi wa Dini kitu ambacho ni kibaya kinawaletea laana
Binafsi. Kwa mustakabali huo ni Vema Basi waziwazi tukaongea sintofaham
hii na kujibu maswali ya kila mwana jamii juu yetu. Siku zote Ufufuo na
Uzima tumekuwa mbele kutolea ufafanuzi kila sentensi inayolenga huduma
hii na kanisa la Mungu kwa ujumla wake hapa Tanzania.
Ifahamike tu wazi kwamba sakata hili tunalisikia sana mitandaoni. Kanisa
kama kanisa hatujui lolote wala Chochote juu ya sakata hili, lilianza
wapi linakwenda wapi na litafikia wapi. Ni Kweli Flora Mbasha na Mumewe
mara Nyingi hupenda kushiriki nasi Kwenye ibaada zetu.
Kanisa limejikita zaidi na huduma ya kiroho. Hatumaanishi kwamba
washirika wetu hawapati mitatizo ya kiutu au kijamii, tunaamini Msingi
Wetu hasa ni Maombi. Na Kama kukiwa Na tatizo la kijamii viko vyombo
husika vya serikali yetu ambavyo ni wajibu wao kutekeleza majukumu Yao.
Tuko katika
maboresho hivi karibuni blog hii itakuwa ni site ambayo itaitwa www.bantutz.com ni katika hatua za kuboresha huduma
zetu za kutoa habari,tutakuja katika muonekano mpya na bora zaidi.
0 comments:
Post a Comment