Kiongozi wa Muslim Brotherhood kunyongwa
21 Juni, 2014 - Saa 09:51 GMT
Wakili mmoja nchini Misri
amesema kwamba mahakama imezingatia hukumu ya kifo cha wanachama
182 wa kundi la Muslim Brotherhood .
Washtakiwa hao ni miongoni mwa watu 700
wanaoshtakiwa kwa kukishambulia kituo kimoja cha polisi katika eneo la
Minya mwaka uliopita.iIongozi wa kundi hilo Mohammed Badie ni miongoni mwa wale waliohukumiwa kifo.
Washtakiwa wengine watano walipewa hukumu nyengeine ya kati ya miaka 15 na 55 huku wengine wakiachiliwa huru.
Hukumu iliotolewa mnamo mwezi Aprili ambapo jaji aliwapatia hukumu ya kifo washtakiwa wote ilizua pingamizi kutoka kwa makundi ya kupigania haki za kibinaadamu.
0 comments:
Post a Comment