Rais wa shirikisho la soka
barani Ulaya ambaye pia ni Makamu wa rais wa FIFA ,Michel Platini
amekashifu Gazeti la Daily Telegraph kwa kuashiria kuwa alikutana na
aliyekuwa Rais wa shirikisho la bara Asia Mohamed bin Hammam muda
mchache kabla ya kura za kuamua mwenyeji wa kombe la dunia la mwaka wa
2022.
Bin Hammam ambaye kwa sasa amepigwa marufuku ya
maisha kwa kushiriki ufisadi ,ana anashtumiwa kwa kuwahonga wanakamati
iliwaipigia kura Qatar kuwa mwenyeji 2022.Makamu huyo wa Rais wa FIFA amemwandikia mhariri wa jarida hilo akifafanua kuwa ‘uvumi hauna misingi na unalenga kumharibia jina.
‘Ni jambo la kuogofya kuwa mazungumzo yangu na mwanachama wa kamati ya FIFA yamegeuzwa kuwa jambo la kitaifa,’ Platini alisema katika barua lililotolewa na UEFA.
Rais huyo wa UEFA alisema kuwa ‘bila shaka’ walikutana na Bin Hammam, mwenzake wa muda mrefu katika FIFA na kiongozi mwenzake katika shirikisho la soka mara nyingi mwaka wa 2010.
Baada ya Qatar kuchaguliwa na bodi ya FIFA kuwa wenyeji wa Kombe la Dunia 2022, Bin Hammam alijaribu kumuondoa Sepp Blatter kama kiongozi wa bodi inayotawala maswala ya soka.
Bin Hammam alijiondoa siku kadhaa kabla ya kupiga kura mnamo mwezi Juni mwaka wa 2011 wakati FIFA ilipokuwa ikijiandaa kumuondoa kwa madai ya kuwahonga wapiga kura wa Caribbean ambapo Blatter alichaguliwa tena.
Bin Hammam alipigwa marufuku maisha kutoshiriki kwa njia yeyote ile shughuli za kandanda.
Tuko katika maboresho hivi karibuni
blog hii itakuwa ni site ambayo itaitwa www.bantutz.com ni katika hatua za kuboresha huduma zetu za
kutoa habari,tutakuja katika muonekano mpya na bora zaidi.
0 comments:
Post a Comment