Mshiriki wa shindano la Big Brother Africa (the chase) 2013, Amir Nando
ameweka wazi kuwa hajawai kuwa na uhusiano ya kimapenzi na mwanadada wa
filamu, Elizabeth Micheal aka Lulu, lakini anakubali sana.
Nando amezungumzia pia mipango yake ya kufanya filamu na mwanadada huyo wa filamu.
“Lulu nishaonana nae, mara mbili mara tatu lakini sina uhusiano nae na
sijawai kuwa na uhusiano nae, ila namkubali sana, mwanamke unajua mzuri,
shepu, mwonekano wake, michezo yake, tunaonana tu ile oya niaje mara
mbili mara tatu. Na proposal mimi, akitaka tukae chini tutengeneze
movie, hicho ndicho nachotaka nifanye, akikubali tutafanya, lakini Lulu
ni mkali, niko tayari kumuoa lakini sijamwambia, Kwa sasa ni mshikaji
wangu tu na napenda kazi zake. Huwa ni mtu ambaye napenda kufuatilia
ishu zake” Alisema Nando.
Tuko katika maboresho hivi karibuni
blog hii itakuwa ni site ambayo itaitwa www.bantutz.com ni katika hatua za
kuboresha huduma zetu za kutoa habari na burudani.Tutakuja katika muonekano
mpya na bora zaidi.Vitu vizuri vipya usivyotarajia utaviona na kufurahia
kupitia www.bantutz.com....
0 comments:
Post a Comment