Facebook

Wednesday, 11 June 2014

Picha:Diamond akiwa studio na Mafikizolo,baada ya kumuomba "collabo"..

 

Kama unakumbuka nilikuhabarisha kuwa Diamond alifanya collable na msanii mwanadada mkubwa kutoka Nigeria anaeitwa Waje, Waje ndio alieomba collabo kwa Diamond na collabo hiyo ilifanyika Nigeria wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kilimo.
Safari hii imekuwa ni wasanii wakubwa wa nje kuomba collablo kwa Diamond tofauti na tulivyozoea wasanii wetu kuomba collablo kujitangaza nje. Mafikizolo kutoka South Africa wameomba collablo na Diamond na baada ya kukutana katika tuzo za MAMA na tayari imeshafanyika katika studio za huko huko South Africa


Jana (June 9) waliingia studio na ku-record collable hiyo



Mafikizolo  ni washindi wa tuzo mbili za MAMA 20114 zilizofanyika Durban, South Africa jumamosi iliyopita

Hatimae mpango huo  wa Mafikizolo wa South Africa ambao ni mastaa wa hit single ya ‘khona’ waliochukua tuzo mbili kwenye MTV Africa music awards 2014 kufanya collabo na Diamond umefanikiwa kwenye usiku wa June 9 2014.
Diamond pamoja na mameneja wake wawili ambao ni Salam na Bab Tale waliongozana mpaka kwenye studio za msanii mkongwe aitwae Oskido ili kurekodi collabo hiyo ya Mafikizolo, kundi la Afrika kusini lililorudi kwenye chati kupitia mikono ya Oskido.
 Mafikizolo waliomba kurekodi wimbo na Diamond baada ya kushawishika kufanya nae collabo hivyo wakaahidi kushughulikia gharama zote za kumuongezea Diamond muda wa kuendelea kukaa South Africa pamoja na kubadili ticket ya ndege ili wakamilishe kazi yao. 
 
 
Tuko katika maboresho hivi karibuni blog hii itakuwa ni site ambayo itaitwa www.bantutz.com ni katika hatua za kuboresha huduma zetu za kutoa habari na burudani.Tutakuja katika muonekano mpya na bora zaidi.Vitu vizuri vipya usivyotarajia utaviona na kufurahia kupitia www.bantutz.com....

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment