Bi Zukile Luyenge
Wabunge wa Afrika Kusini
wamelalamika juu ya chakula kinachopikwa katika mgahawa ulio katika
majengo ya bunge wakisema kuwa kinawafanya kunenepa kupita kiasi.
Wabunge hao wamelalamika juma hili kwamba wengi
wao huingia katika bunge hilo wakiwa wakonde na wadogo lakini wanaishia
kunona kwa sababu ya vyakula visivyokuwa na afya vinavyopatikana katika
mkahawa wa bunge.''Sisi wabunge huingia katika bunge hili tukiwa na umbo nzuri wadogo na wa kupendeza, lakini muhula wetu unapokwisha , tutakuwa wanene kupindukia,'' alisema mbunge mmoja wa chama cha ANC ,Sheila Sithole.
Mbunge mwenzake Zukile Luyenge anakubaliana na kauli hiyo: ''Kila chakula kinachouzwa hapa kina mafuta mengi na proteni nyingi.''
Wanasiasa wanapofanya mikutano yao wakati wa mchana hulazimika kula Sambusa, Sausage au nyama ya Kondoo kati ya vyakula vingine vya mafuta vinavyouzwa kwenye mkahawa huo.
Wabunge wanasema mkahawa huo unauza Sambusa, Sausage na nyama ya aina aina
Mnamo mwaka 2012, waziri wa afya nchini humo Aaron Motsoaledi, alianza kunenepa sana kwa kubugia chakula hicho ingawa alinukuliwa akisema , ''tatizo na kazi yao ni kwamba kuna chakula kila mahali.''
Hata hivyo mmoja wa wabunge hao anawashauri wenzake kuanza kufanya mazoezi ili kupunguza uzito.
Bi Sheila Sithole alisema, “Tulichogundua kuhusu vyakula vya hapa bungeni ni kwamba kila chakula kina mafuta na protini kwa wingi. Kwa kawaida, hufai kula mafuta mengi na Protini kwa wakati mmoja.”
“Kuna vyakula mbalimbali lakini vina mafuta, ikiwemo Samaki. Afadhali kula nyama kila wakati kuliko kula Samaki iliyopikiwa hapa bungeni,” alisema mbunge huyo.
Sithole amewataka wabunge kufanya mazoezi katika jumba la kufanyia mazoezi lililoko katika majengo ya bunge, kama anavyofanya mwenyewe iwapo watataka kuepuka unene.
Tuko katika maboresho hivi karibuni
blog hii itakuwa ni site ambayo itaitwa www.bantutz.com ni katika hatua za
kuboresha huduma zetu za kutoa habari na burudani.Tutakuja katika muonekano
mpya na bora zaidi.Vitu vizuri vipya usivyotarajia utaviona na kufurahia
kupitia www.bantutz.com....
0 comments:
Post a Comment