Facebook

Tuesday, 3 June 2014

Raia 130,000 wa DRC wafukuzwa Brazaville



Zaidi ya wakimbizi 130,000 kutoka Jamhuri ya Demokrasia ya Congo wamefukuzwa kutoka Congo Brazaville tangu mwezi Aprili.
Wengi wao sasa wanaishi katika kambi za muda nchini DRC.
Serikali ya Brazzaville imesema kuwa watu hao walikuwa wahamiaji haramu lakini wengi wao wamekanusha hili wakisema kuwa wameteswa sana na polisi wa Brazaville.
Umoja wa maaifa umetoa wito kwa Congo kukoma kuwafukuza watu hao.
Hapo Jumatatu ujumbe kutoka pande zote mbili ulikutana mjini Kinshasa nchini DRC kujaribu kutafuta suluhisho.

Maelfu ya waliohamia kambi hizo za muda za DRC waliishi nchini Brazaville maisha yao yote na sasa wamepoteza kila kitu walichokuwa nacho.
Wamedai kuwa polisi wa Brazaville waliwapiga, kuwabaka na hata kuwaua baadhi ya watu walioaminiwa kuwa raia wa DRC wakati wa msako wao.

Huu ni unyama

Upande wa DRC umelalamikia hatua hii na kusema kuwa Brazaville imekiuka haki za binadamu.
Richard Muye ni waziri wa mambo ya ndani wa DRC .Amesema '' Mbona sasa wanawafukuza tena kwa wingi hivi bila kujali haki zao? Wanawatesa watu wote, wake waume na hata watoto.''

Brazaville yajitetea

Lakini waziri mwenzake kutoka upande wa Brazaville Raymond Zéphirin Mboulou amekanusha kuwafukuza wakongomani 130,000. Amesisitiza kuwa ni 2000 pekee waliofukuzwa kwa lazima nchini humo, na hiyo pia ni kwasababu walikuwa wahalifu.
"Walifanya uhalifu wa kuchukiza. Wizi, ubakaji ukahaba na mengine. Wameharibu mitaa yetu. Na hawakaribishwi hapa tena kwasababu hao wahamiaji ndio wanaowahangaisha raia wetu usiku na mchana."
Waziri huyo ameongeza kuwa wale wengine 128,000 walioondoka walifanya hivyo kwa hiari yao.



Tuko katika maboresho hivi karibuni blog hii itakuwa ni site ambayo itaitwa www.bantutz.com ni katika hatua za kuboresha huduma zetu za kutoa habari,tutakuja katika muonekano mpya na bora zaidi.

0 comments:

Post a Comment