Mmoja wa waasisi wa mtandao wa kijamii wa Instagram, amesema kuwa sheria zake kuhusu picha za uchi hazimbagui mtu yeyote.
Kampuni hiyo imekosolewa vikali kwa kwa kuondoa picha za wanawake walio nusu uchi kwenye mtandao huo.Masharti ya matumizi ya mtandao wenyewe, yanasema: 'Mtu haruhusiwi kuweka picha za watu walio nusu uchi na picha zenye mada ya ngono. ''
Matamshi yake yanakuja baada ya mwanawe muigizaji maarufu, Bruce Willis, Scout Willis kuweka picha yake kwenye mtandao huo akiwa nusu uchi bila kitu kifuani.
Muimbaji Rihanna, ambaye alikuwa na wafuasi milioni 1.3 aliunga mkono kampeini hiyo kabla ya kufunga akaunti yake.
Wamiliki wa mtandao huo wanasema sheria zinapaswa kufuatwa na kila mtu awe mtu mashuhuri au vinginevyo.
"lengo letu ni kuhakikisha kuwa Instagram, ni mahala salama kwa kila mtu , awe maarufu au la. ''
"tunapaswa kuwa na sheria na kuhakikisha kuwa kila mtu anafuata sheria hizo. Bila shaka tunapata changamoto nyingi lakini tutnaedneklea kusisitiza umuhimu wa sheria kufuatwa, '' alisema Systrom
Huku umaarufu wa mtandao huo ukiendelea kuimarika, mtandao huo umekosolewa kuhusiana na baadhi ya picha zinazochapishwa humo . Pia mtandao wenye umebana baadhi ya maneno yanayohusiana na madawa ya kulevya.
Instagram ilinunuliwa na Facebook mwaka 2012.
Tuko katika maboresho hivi karibuni blog hii itakuwa ni site ambayo itaitwa www.bantutz.com ni katika hatua za kuboresha huduma zetu za kutoa habari,tutakuja katika muonekano mpya na bora zaidi.
0 comments:
Post a Comment