Meneja Wa Arsenal Arsene Wenger yuko tayari kutumia kitita cha paundi milioni 100 za usajili baada ya yeye mwenyewe kusaini mkataba wa miaka mitatu (Daily Mail),
QPR wanataka kumsajili beki wa Man City Joleon Lescott
(Daily Mirror),
klabu ya Montpellier ya Ufaransa imeiambia Newcastle
lazima watoe paundi milioni 12 kumsajili kiungo mshambuliaji Remy
Cabella (Guardian),
Rais wa Barcelona Josep Maria Bartomeu amezionya
Arsenal na Manchester United kuwa Cesc Fabregas hauzwi (Metro),
Valencia
watapambana vikali na Liverpool na Everton kusaka saini ya Thorgan
Hazard, mdogo wake Edin Hazard wa Chelsea (Daily Express),
Manchester
United huenda wakawazidi kete Liverpool katika kumsaini kiungo wa
Ukraine Yevhen Konoplyanka kutoka FC Dnipro (Talksport),
Demba Ba
anafanya mazungumzo na Besitkas kuhamia klabu hiyo ya Uturuki kwa
paundi milioni 8 (Daily Mirror),
Meneja mpya wa Barcelona Luis Enrique
anataka Sergio Aguero wa Manchester City kuwa mchezaji wake wa kwanza
kumsajili. Barcelona iko tayari kutoka Euro milioni 38 (Sport),
Mshambuliaji wa PSG Edison Cavani hatosikiliza dau la Man United kwa
sababu United hawachezi Champions League msimu ujao, na atasalia
Ufaransa (L'Equipe),
Liverpool inajiandaa kutoa paundi milioni 20
kumnunua Alexis Sanchez kutoka Barcelona.
NA HATIMAYE...Takriban watu 700 katika jimbo la Catalan la Spain wamewapa jina la Messi, mbwa na paka wao. Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa, ni watu 10 tu wamewapa wanyama wao jina la Ronaldo wa Real Madrid. Share tetesi hizi na wapenda soka wote. Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Adios!
Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com kupata tetesi mbalimbali za usajili barani Ulaya ikiwa dirisha la usajili linafunguliwa hivi karibuni.
0 comments:
Post a Comment