Kuna baadhi ya binadamu wana roho mbaya zaidi ya wanyama wakali wa
mwituni na ukisimuliwa matukio waliyofanya unaweza kujiuliza kama kweli
ni binadamu au ‘mashetani’!
Siku mbili baada ya kuripotiwa habari ya kusikitisha ya wasichana wawili
ndugu wa nchini India waliobakwa na baadae kunyongwa, mtandao wa
MailOnline umeripoti tukio la ubakaji alilofanyiwa msichana mdogo mwenye
umri wa miaka 15 na wanaume zaidi ya 38 nchini Malaysia.
Taarifa zinaeleza kuwa tukio hilo limefanyika Kaskazini mwa Kelantan,
Malaysia, May 20 ambapo msichana huyo alienda sehemu fulani kukutana na
rafiki yake mwenye umri wa miaka 17 lakini alijikuta akipelekwa kwenye
jumba bovu wasiloishi watu.
Akiwa kwenye jumba hilo, msichana huyo alibakwa kwa zamu na wanaume hao
ambao miongoni mwao ni kundi la watu wanaojihusisha na matumizi ya
madawa ya kulevya.
Msichana wa miaka 17 ambaye ni rafiki ya msichana huyo anasadikika kuwa
ndiye aliyemtenezea mazingira ya kuingia mikononi mwa watu hao wanyama
japo polisi wamesema wanaendelea na uchunguzi ili waweze kufahamu kama
kweli msichana huyo alihusika kupanga njama ama na yeye alibakwa.
Polisi wa Malaysia wamewakamata watuhumiwa 13 hadi sasa na kwamba kati ya hao yupo baba na watoto wake wawili wa kiume.
0 comments:
Post a Comment