
Mshambuliaji wa Chelsea Romelu Lukaku amekataa kwenda West Ham kwa mwaka wa pili sasa, lakini huenda akajiunga na Wolfsburg ya Ujerumani (Daily Mirror),
Manchester United sasa wamemgeukia kiungo wa Bayern
Munich, Bastian Schweinsteiger baada ya
kushindwa kumpata Thomas Muller (Daily Star),
Arsenal wapo tayari kutoa
pauni milioni 5 kwa kipa Pepe Reina (Metro),
Arsenal pia wanataka
kumsajili beki Bressan kutoka Gremio ya Brazil (Daily Express),
Arsene
Wenger pia anakaribia kukamilisha usajili wa Carlos Vela kutoka Real
Sociedad (Sun),
Liverpool wana imani wataweza kumsajili Max Meyer kutoka
Schalke na kuwapiku Arsenal na Chelsea (Daily Express),
kiungo wa
Barcelona, Alex Song ameambiwa yuko huru kuondoka Nou Camp, huku
Manchester United wakimfuatilia mchezaji huyo wa zamani wa Arsenal
(Talksport),
Rais wa Real Madrid Florentino Perez ameruhusu klabu yake
kumfuatilia Ramires wa Chelsea (Marca),
Paris St-Germain itamfuatilia
kipa Petr Cech iwapo Chelsea hawatamhitaji (Le Figaro),
Atlètico Madrid
wanafikiria kutoa pauni milioni 18 kumsajili kiungo wa Arsenal Santi
Cazorla (As.com).
Share tetesi hizi na wapenda soka wote. Tetesi
nyingine kesho.
Hivi sasa
tunahamia katika site yetu mpya inayoitwa www.bantutz.com
ni katika kuboresha huduma zetu za kutoa habari za uhakika na burudani.
0 comments:
Post a Comment