Manchester United wamerejea tena kumfuatilia kiungo wao wa zamani Paul
Pogba, anayechezea mabingwa wa Italia, Juventus- ambaye bei yake sasa ni
takriban pauni milioni 60 (Sunday Express),
Didier Drogba huenda akarejea
Chelsea kutoka Galatasaray ya Uturuki (Sunday Mirror),
Southampton
watafanya mazungumzo wiki ijayo na Ronald Koeman ambaye huenda akachukua
nafasi ya Mauricio Pochettino (Mail on Sunday),
Manchester City
watalipa pauni milioni 25 kumpata beki wa Real Madrid Pepe, ili
kusaidiana na Vincent Kompany (Daily Star Sunday),
Meneja wa Man United,
Louis van Gaal amezungumzia kupendezwa na Arturo Vidal, na kukiri kuwa
ni mchezaji ambaye "angependa kumnunua". Vidal kutoka Chile anayechezea
Juventus, anasakwa na timu kadhaa ikiwemo Real Madrid, Barcelona na
Chelsea (Mail on Sunday),
Arsenal wanatazamia kumsaini tena Carlos Vela
kutoka Real Sociedad kwa pauni milioni 3.25 (Sunday Sun),
Arsenal pia
wanamtazama kipa wa Nice, David Ospina, na huenda wakamfuatilia, lakini
itategemea kiwango atakachoonesha wakati wa Kombe la Dunia (Sunday
Mirror)
Real Madrid watatazama dau kuanzia pauni milioni 40 kwenda juu
kwa Angel Di Maria. Manchester United na Arsenal zinamtamani mchezaji
huyo kutoka Argentina (L'Equipe),
Paris St-Germain wanatazamia kuwazidi
kete Arsenal, Liverpool na Manchester United katika kumsajili Antoine
Griezmann, baada ya Eden Hazard kuhakikisha kuwa haondoki Chelsea (Daily
Star)
Carlos Vela ameiambia klabu yake ya Real Sociedad kuwa amepata
mkataba mnono kutoka Atlètico Madrid (Marca).
Share tetesi hizi na
wapenzi wote wa kandanda. Tetesi nyingine kesho, tukijaaliwa. !
Tuko katika maboresho hivi karibuni
blog hii itakuwa ni site ambayo itaitwa www.bantutz.com ni katika hatua za
kuboresha huduma zetu za kutoa habari na burudani.Tutakuja katika muonekano
mpya na bora zaidi.Vitu vizuri vipya usivyotarajia utaviona na kufurahia
kupitia www.bantutz.com....
0 comments:
Post a Comment