Mtaalamu mashuhuri wa maradhi ya
Ki-akili ya dementia ambayo huathiri uwezo wa kufikiri, Daktari Dennis
Gillings, amejitokeza na kuzungumzia kile anachokiita, mwendo wa Kobe
katika taratibu ya kupata tiba mpya ya ugonjwa huo. Ugonjwa huo wa akili
unawaathiri zaidi ya watu milioni 4 kote Duniani.
Daktari Gillings ambaye aliteuliwa na waziri
mkuu wa Uingereza mwaka jana amesema ahadi zilizotolewa na mataifa
manene yenye uchumi mkubwa duniani G8 kutafuta tiba ya ugonjwa huo
kufikia mwaka 2025 haziwezi kutimizwa bila kuwekeza zaidi katika
utafiti.Miezi sita baada ya ahadi hizo kutolewa wataalam kutoka maeneo mbalimbali duniani wanakutana London ili kujadili hatua zinazohitajika kuimarisha utafiti na majaribio ya dawa za kutibu ugonjwa huo.
Daktari Gillings anasema majaribio ya dawa hizi yanapaswa kudhibitiwa kuambatana na utaratibu wa majaribio ya dawa zingine.
Serikali ya Uingereza inatarajiwa kuwasilisha ripoti kuhusu ugonjwa huo nchini humo ambapo watu laki nane wameathirika. Wanasayasi pia watatoa ripoti itakayoangazia uhusiano wa Ugonjwa wa dementia na lishe.
0 comments:
Post a Comment