Facebook

Sunday, 8 June 2014

Yule mganga wa Ghana aendelea kumtengeneza Cristiano Ronaldo!

Maneno ya mganga wa kienyeji wa Ghana, Nana Kwaku Bonsam, yameanza kudhihirika baada ya uongozi wa timu ya taifa ya Ureno kuthibitisha taarifa za mshambuliaji Cristiano Ronaldo, kutokuwa sehemu ya kikosi cha timu ya taifa ya Ureno ambacho juzi kilicheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Mexico.

Nana Kwaku Bonsam, amesema yeye ndiye anayemroga nahodha huyo wa timu ya taifa ya Ureno, ili asicheze mchezo wa kundi la saba katika fainali za kombe la dunia ambapo timu ya taifa ya Ureno itapambana na timu ya taifa ya Ghana, Black Stars. 


Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Ureno Paul Bento alisema pamoja na kutarajia kumkosa Ronaldo katika mchezo wa juzi  wa kirafiki, bado hajafahamu ni lini mshambuliaji huyo atakuwa fit kwa ajili ya kujiunga na wenzake. 


Mshambuliaji huyo wa klabu ya Real Madrid anasumbuliwa na maumivu ya mishipa fulani laini katika mguu wake, ambapo kwa mara ya mwisho alionekana uwanjani wakati wa mchezo wa hatua ya fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya walipocheza dhidi ya Atletico Madrid.




Tuko katika maboresho hivi karibuni blog hii itakuwa ni site ambayo itaitwa www.bantutz.com ni katika hatua za kuboresha huduma zetu za kutoa habari na burudani.Tutakuja katika muonekano mpya na bora zaidi.Vitu vizuri vipya usivyotarajia utaviona na kufurahia kupitia www.bantutz.com....

0 comments:

Post a Comment