Facebook

Friday, 22 August 2014

Tetesi za usajili katika magazeti mbalimbali barani Ulaya na BantuTz SPORTS


>Juventus na Roma wanataka kumsajili beki wa
kati wa Manchester City Matija Nastasic, 21,
huku Newcastle na West Ham wakimtaka beki
wa kulia wa Man City Micah Richards, 26,
(Manchester Evening News),

>Manchester
United wanaongoza mbio za kumsajili winga
wa Real Madrid Angel Di Maria, 26 baada ya
mabingwa wa Ufaransa PSG kuamua kujitoa
(Daily Star),

>Lakini Di Maria huenda asiende
United kwa sababu Louis van Gaal hataki
kukwaza ukuaji wa Adnan Januzaj, 19, (Daily
Express),

>Tottenham wanajiandaa kutoa pauni
milioni 11 kumchukua mshambuliaji wa QPR
Loic Remy, 27, (Daily Star),

>Arsenal
wanafikiria kupanda dau kumchukua beki wa
West Ham Winston Reid, 26, ambaye
mkataba wake unamalizika msimu ujao (Daily
Star),

>Hull City wameongeza dau kumchukua
mshambuliaji wa Blackburn Jordan Rhodes,
24 (Daily Mail),

>kiungo wa Manchester
United Anderson, 26, huenda akahamia
Sporting Lisbon kwa pauni milioni 5.5 (Daily
Express),

>Meneja mpya wa Southampton Ronald
Koeman amesema kiungo wake Morgan
Schneiderlin, 24 hauzwi kwa bei yoyote
(London Evening Standard),

>Beki wa QPR Rio
Ferdinand, 35, anataka kuwa meneja wa
England akistaafu kucheza (Daily Mail),

>Newcastle United wana uhakika nahodha wao
msaidizi Cheick Tiote, 28 hatoondoka licha
ya timu nyingi kumnyatia (Sunderland Echo),

>Meneja wa Arsenal Arsene Wenger anaamini Jack
Wilshere, 22, anatolewa kafara kwa England
kushindwa kufanya vizuri katika Kombe la
Dunia (Sun),

>Wakati huohuo Aaron Ramsey,
23, ana uhakika Arsenal wataweza kupambana
"kwa misuli" na Manchester City na Chelsea
msimu huu (Sky Sports),

>Barcelona
wamefanya jaribio la kushangaza la kumtaka
Angel Di Maria kutoka Real Madrid. Real
walifikiria dau la pauni milioni 48 lakini
mazungumzo ya awali yalivunjika baada ya
Los Bloncos kutotaka kuwauzia mahasimu
wao (Sport),

>Napoli wanamtazama Fabio
Borini wa Liverpool, ambaye kuwasili kwa
Mario Balotelli huenda kukasaidia kufanikisha
uhamisho wake (Tuttosport),

>Dau la
Manchester United kumtaka Nicolas Gaitan
limekataliwa na Benfica (Record),

>Arsenal
wanafikiria kumchukua William Carvalho
kutoka Sporting, huku Sami Khedira anaweza
kwenda Emirates iwapo atashusha madai ya
mshahara mkubwa (Daily Telegraph),

>AC
Milan wanajiandaa kumtaka mshambuliaji wa
Tottenham Roberto Soldado kuziba pengo la
Mario Balotelli anayeelekea Liverpool. Spurs
watamruhusu Soldado kuondoka na nafasi
yake kuzibwa na Loic Remy kutoka QPR (Daily
Mail),

>Manchester United na Zenit St
Petersburg wapo tayari kupambana kumwania
kiungo wa Inter Milan Fredy Guarin (Corriere
dello Sport),

>Barcelona wanatumaini
kukamilisha usajili wa Marco Reus kutoka
Borrusia Dortmund.
Maafisa wa Bayern wana wasiwasi kuwa
huenda mchezaji huyo tayari amekubali
kujiunga na Catalans ambao huenda
wakafungiwa kusajili (Mundo Deportivo).

Endelea kutembelea www.bantutz.com uweze kupata habari zinazogusa katika kila myanja ya maisha ya mwanadamu.

Related Posts:

  • Tetesi zote za Usajili barani Ulaya siku ya leo.Winga wa England Raheem Sterling, 20 hana tatizo na uwezekano wa kuhamia Manchester United kutoka Liverpool, ingawa mchezaji huyo ana wasiwasi kuhusu jinsi uhamisho huo utakavyopokelewa, kwa kuzingatia uhasama baina ya timu h… Read More
  • Man City yamuwekea dau Alex SongManchester City imeonyesha nia ya kupata huduma ya mchezaji wa Barca Alex Song ambaye msimu huu alikuwa akicheza kwa mkopo timu ya Westham inayoshiriki.Alex aliyerudi nyumbani Barcelona anaweza kuuuzwa jumla na kujiunga na … Read More
  • Dante atakiwa Man United.Mchezaji wa kimataifa wa Brazil Dante anatakiwa na timu ya Manchester United kwenda Old Trafford msimu huu. Timu ya Manchester ipo tayari kumpa mkataba mchezaji huyo kujiunga na mashetani hao.Lakini mchezaji mwenyewe Dante am… Read More
  • Skrtel akataa kusaini kataba mpya Liverpool.  Beki wa klabu ya Liverpool Martin Skrtel amefichua kuwa bado hajasaini mkataba mpya na klabu hiyo kama ambavyo inaripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari nchini England pamoja na nyumbani kwao huko Slovakia. Skr… Read More
  • Everton yamnasa Tom Cleverley.Everton watamsajili Tom Cleverley kwa mkataba wa miaka mitano wakati mkataba wake na Manchester United utakapomalizika Julai 1. Mchezaji huyo wa kimataifa wa England atakuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa msimu huu na meneja R… Read More

0 comments:

Post a Comment