Vyombo vya habari vya Nigeria vimeripoti habari ya mtu mmoja aliyekutwa
amefia kaburini kwamba alikubwa na umauti wakati akifanya jaribio la
kufukua kaburi ili aibe fuvu la marehemu kwa ajili ya matumizi ya mambo
ya kishirikina.
Kwa mujibu wa Saturday Tribune la Nigeria, tukio hilo limetokea katika
mji wa Ilobu eneo oa Osun ambapo mtu huyo alikutwa akiwa amekufa huku
nusu ya mwili wake ukiwa umeingia kaburini.
Mmoja wa wakazi wa eneo hilo ameeleza kuwa kijana huyo alikuwa na
marafiki zake wengine waliokuwa wanafanya tukio hilo kwa lakini baada ya
kuona mwenzao amenaswa ndani ya kaburi wakakimbia na kumuacha huku wao
wakiwa salama.
“Mwili wake ulikutwa majira ya saa kumi na mbili na nusu asubuhi na
kichwa chake kilikuwa kimefunikwa na tope. Wakazi wa eneo hili
waliripoti polisi na walikuja baadae wakautoa mwili wake na kuuweka
kwenye gari lao na kuondoka nae.” Alisema mkazi wa eneo hilo.
Saturday Tribune iliongea na kamishina wa Jeshi la Polisi wa eneo la
Osun, Ibrahi Maishanu ambaye alieleza kuwa polisi watafanya uchunguzi wa
kina kufuatia tukio hilo kufahamu nini hasa kilikuwa chanzo cha kifo
chake. Na kwamba polisi hawajathibisha kuwa tukio hilo linatokana na
masuala ya kishirikina
Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com uweze kujua matukio mbalimbali yanayotokea duniani
Monday, 19 May 2014
Afia Kaburini Baada ya Kunaswa na Kitu Akijaribu Kufukua ili Aibe Fuvu
Related Posts:
"Hatujampigia magoti Zitto Kbwe"-Ukawa "Habari inayoenezwa kuwa viongozi wakuu wa UKAWA na hata waandamizi nikiwemo mimi, eti tumembembeleza mhe. Zitto Kabwe ili aunge mkono mikutano ya UKAWA kuzunguka nchi siyo taarifa zenye ukweli wowote.Mhe Zitto ha… Read More
Busara za Nyerere na Karume hakuna wa kuziendeleza...................?????? Mwl Nyerere na Sheikh Karume wakinywa Fanta bariiidi tena kwa mrija.....Hii ni kutokana na uzalendo waliokuwa nao waasisi hawa wa muunagano bila kujikweza wala kujilimbikizia mali tabia inayofanywa na viongozi wa sasa we… Read More
Hii ndio Orodha ya matajiri waliofanikiwa kutokana na Biashara ya mtandao {Network marketing}........fuatilia hapa.......... Rank ya Dunia Jina Kampuni Kipato/mwezi kipato/mwaka 1 Holton Buggs OrganoGold $1,200,000 $14,400,000 2 Angela Liew and Ryan Ho NuSkin $1,100,000 $13,200,000 3 Dexter & Birdie Yager Amway $1,000,000 $12,000,000 … Read More
Soma hapa barua ya Jeshi la Polisi inayowazuia Upinzani (Ukawa) kutokufanya maandamano.........fuatilia hapa............ Baada ya kugoma kuendelea kuhudhuria vikao vya bunge la katiba Dodoma, Umoja wa katiba ya Wananchi (UKAWA) unaoongozwa na Profesa Ibrahim Lipumba na Freeman Mbowe ulitangaza kufanya mkutano Zanzibar Jumamosi ya … Read More
Je unamfahamu askari Polisi aliyekamatwa ameiba mtoto ......fuatilia hapa..........!!!! POLISI WA KIKE AIBA MTOTO MCHANGA Jeshi la polisi Mbeya limemkamata Askari polisi mwanamke wa Dar es salaam kwa tuhuma za kumuiba mtoto mchanga wa siku ambae aliibwa toka April 6 … Read More
0 comments:
Post a Comment