Facebook

Monday, 19 May 2014

Mascherano "Ubabe wa Barcelona umefikia kikomo"

381124_heroaKIUNGO wa Barcelona, Javier Mascherano amekiri kuwa ufalme wa klabu hiyo katika soka la Hispania na Ulaya kwa ujumla umefika kikomo.
Wakatalunya walishindwa kutetea ubingwa wao wa La Liga baada ya kushindwa kuwafunga Atletico Madrid kwenye uwanja wa Camp Nou jana usiku na kumpa nafasi Diego Simeone kunyakua `ndoo`.

Atletico Madrid licha ya kuwabania Barca kutetea taji lao, pia waliwatoa katika hatua ya robo fainali ya UEFA.

Mambo yalikuwa mabaya zaidi kwa Barca baada ya kufungwa na Real Madrid katika fainali ya Copa del Rey na sare ya jana imewafanya wamalize msimu bila kombe.

Mascherano anaamini kufanya vibaya msimu huu kunadhihirisha kuwa ufalme wa Barcelona umefikia kikomo na yanatakiwa mabadiliko makubwa, lakini alikaa kimya kuhusu hatima yake ya baadaye klabuni hapo.

“Kuzungumzia hatima ya Mascherano ni jambo dogo sana, kinachotakiwa ni kuizungumzia Barcelona. Ufalme umekwisha.” Aliambia Barca TV.

“klabu itafanya maamuzi na mabadiliko, lakini lazima tukubali kuwa msimu huu haukuwa mzuri”.

Kocha Tata Martino amethibitisha kuondoka Barcelona majira ya kiangazi mwaka huu, huku Luis Enrique akitarajiwa kurithi mikoba yake.

0 comments:

Post a Comment