Ryan Giggs amekubali kuwa msaidizi wa Louis van Gaal, Manchester United.
RYAN
Giggs yuko tayari kukubali ofa ya Louis van Gaal kuwa msaidizi wake
katika klabu ya Manchester United – lakini makocha wenzake, Paul
Scholes, Nicky Butt na Phil Neville bado wanaona giza mbele yao juu ya
maisha yao ya baadaye klabuni hapo.
Giggs
aliyeteuliwa kuwa kocha mkuu wa muda baada ya kutimuliwa kwa David
Moyes kwasasa yuko likizo baada ya kukutana na Van Gaal.
Inafahamika kuwa mazungumza yalikwenda vizuri na Van Gaal alikubali kuwa Giggs awe msaidizi wake.
Pia Van Gaal will atamleta Franz Hoek katika nafasi ya kocha wa makipa pamoja na kocha wa viungo Jos van Dyk na Max Reekers.
Man United
inatarajia kumtangaza Mholanzi huo wakati wowote kutoka sasa na
ilitakiwa watangaze alhamisi ya wiki hii, lakini waliahirisha ili
kutomharibia Van Gaal katika maandalizi yake ya mechi ya kirafiki kati
ya timu ya taifa ya Uholanzi na Ecuador.
Giggs
atatangazwa pamoja na van Gaal, lakini kocha mpya Mholanzi anataka
kumleta mholanzi mwingine na inaonekana Rene Meulensteen anaweza kurudi
tena Man United baada ya kuondoka wakati Sir Alex Ferguson alipostaafu.
Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com uweze kujua kila kianachokuwa kinaendelea katika sakata hili ndani ya timu ya Manchester United fc
0 comments:
Post a Comment