Wiki jana Misri ilifanya dhuluma za kingono kuwa uhalifu ambao adhabu yake ni miaka 5 jela
Wanaume saba wamekamatwa nchini
Misri, baada ya kushukiwa kuwadhulumu kiongono wanawake katika sherehe
za Jumamosi za kumkabidhi rasmi mamlaka Rais Abdul Fattah al Sisi.
Hatua ya kuwakamata wanaume hao, inakuja baada
ya kanda ya video kusambazwa kwenye internet ikionyesha mwanamke
akivuliwa nguo na kuvamiwa na genge la wanaumeHaijulikani ikiwa kanda hiyo ilinaswa, lakini walioshuhudia kitendo hicho alisema kwambwa unyama huo ulitokea Jumapili usiku.
Wiki jana maafisa wa utawala nchini Misri, waliharamisha dhuluma za kingono na kuufanya uhalifu kwa mara ya kwanza adhabu yake ikiwa miaka mitano jela kwa watakaopatikana na hatia.
Tuko katika maboresho hivi karibuni
blog hii itakuwa ni site ambayo itaitwa www.bantutz.com ni katika hatua za
kuboresha huduma zetu za kutoa habari na burudani.Tutakuja katika muonekano
mpya na bora zaidi.Vitu vizuri vipya usivyotarajia utaviona na kufurahia
kupitia www.bantutz.com....
0 comments:
Post a Comment