Facebook

Monday, 16 June 2014

Misri waiomba YouTube kuondoa video ya mwanamke aliyebakwa

Waandamanaji wakiwa wameshika mabango kupinga kuonyeshwa kwa video ya mwanamke kubakwa Misri.
Waandamanaji wakiwa wameshika mabango kupinga kuonyeshwa kwa video ya mwanamke aliyebakwa Misri.
Misri imeiomba YouTube kuondoa video ya mwanamke anayedhalilishwa kijinsia wakati wa mkutano kwenye medani ya Tahrir akimuunga mkono rais mpya mteule.
Msemaji wa Rais Abdul Fattah al-Sisi alisema ombi hilo lilifanywa na ubalozi wa Misri mjini Washington.
Mwanamke huyo ameomba kuondolewa kwa video hiyo wakati Sisi alipomtembelea hospitali siku ya Jumatano, alisema.
YouTube hawajajibu maombi ya taarifa hiyo.
Video hiyo, ambayo inamuonyesha mwanamke huyo akivuliwa nguo na kuvamiwa katika medani ya mji mkuu ya Tahrir, iliyorushwa wiki hii.
Msururu wa mashambulio wakati wa sherehe za hivi karibuni umesababisha jazba.


Tumehamia katika site hii mpya na bado tuko katika maboresho,hii ni katika hatua za awali kabisa kuiboresha site yetu na utoaji wa habari na burudani.Vitu vingi vitaonekana katika site hii mpya hivi karibuni.Endelea kutembelea www.bantutz.com

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment