Raia huyo wa Ujerumani, 45, ataendelea na matibabu kwenye eneo ambalo halijatajwa, familia yake ilieleza kwenye taarifa.
Schumacher aliwekwa kwenye hospitali ya magonjwa ya coma baada ya kupata majeraha makali kichwani aliyoyapata kwenye ajali ya mcezo wa kuteleza barafuni katika vilima vya Ufaransa Desemba 29.
Familia yake imewashukuru watu waliotuma ujumbe wa kumuunga mkono, wanasema: “Tuna uhakika ilimsaidia sana”.
Pia walisifia kazi nzuri ya madaktari wa hospitali ya Grenoble, kusini-mashariki mwa Ufaransa.
Madaktari walimuweka bingwa huyo mara saba wa mbio za magari kwenye coma kupunguza kuvimba kwa ubongo wake.
Tumehamia
katika site hii mpya na bado tuko katika maboresho,hii ni katika hatua za awali
kabisa kuiboresha site yetu na utoaji wa habari na burudani.Vitu vingi
vitaonekana katika site hii mpya hivi karibuni.Endelea kutembelea www.bantutz.com
0 comments:
Post a Comment