MTANGAZAJI wa maarufu wa runinga Bongo, Peniel Mungilwa ‘Penny’
amefunguka kuwa ugonjwa uliompiga juzikati ulikuwa ‘serious’ kiasi cha
kuona ni Mungu tu amemwokoa.
Akichezesha taya na paparazi wetu, Penny alisema anamshukuru Mungu
anaendelea vizuri kwani alikuwa na hali mbaya baada ya kubanwa na
ugonjwa wa Athma kwa siku tatu nzima akiwa anasaidiwa kupumua na mashine
ya oxygen.
“Ukweli nilikuwa na hali mbaya huwa nasumbuliwa na Athma mara kwa mara
lakini naweza kubanwa kwa siku moja ila ya safari hii imekuja kwa nguvu
sana kwa sababu ilikuja na mafua makali jambo lililosababisha nilazwe
kwa siku tatu katika Hospitali ya AAR huku nikipumua kwa kutumia
mashine, kweli Mungu ni mkubwa, ninaendelea vizuri,”
Tumehamia
katika site hii mpya na bado tuko katika maboresho,hii ni katika hatua za awali
kabisa kuiboresha site yetu na utoaji wa habari na burudani.Vitu vingi
vitaonekana katika site hii mpya hivi karibuni.Endelea kutembelea www.bantutz.com
0 comments:
Post a Comment