Utabiri wa Ngamia - Ureno kuisambaratisha Ujerumani
Baada ya Pweza kutabiri matokeo katika fainali za kombe la dunia zilizofanyika nchini Ujerumani mwaka 2006.Huku akitabiri mechi nyingi na matokeo yake kuwa ya kweli.
Lakini Fainali za mwaka huu huko Saudi Arabia ameibuka Ngamia ambaye amekuwa akitabiri matokeo mbalimbali ya mechi za kombe la dunia nchini Brazil.
Akiwa amekwisha tabiri matokeo ya mechi ya ufunguzi na kuwa sahihi,Brazil ikaibuka na ushindi wa magoli 3-1,akatabiri tena mechi kati ya Spain na Uholanzi hatimaye Uholanzi ikashinda magoli 5-1,England dhidi ya Italy,Italy ikashinda.Na hapo jana akatabiri matokeo kati ya Argentina na Bosnia Herzgovina,Argentina ikaibuka na ushindi wa Magoli 2-1.
Leo hii Ngamia ametabiri matokeo kati ya mahasimu wakubwa Ujerumani watakaopambana na Ureno majira ya saa 1 kwa saa za Afrika Mashariki huku akitabiri Ureno kushinda mechi hiyo.
Huku Ureno ikiwa inamtegemea staa wake,Cristian Ronaldo ambaye ni mchezaji bora wa dunia huku akiwa na hatihati ya kuukosa mchezo huo.
Haya sasa wale wazee wa kuweka mizigo haina haja ya kujishauri mara mbilimbili Ngamia kashawasaidia......
Tumehamia
katika site hii mpya na bado tuko katika maboresho,hii ni katika hatua za awali
kabisa kuiboresha site yetu na utoaji wa habari na burudani.Vitu vingi
vitaonekana katika site hii mpya hivi karibuni.Endelea kutembelea www.bantutz.com
0 comments:
Post a Comment