
Madaktari wamesema wanaamini wanauwezo wa kuokoa maisha ya watoto hao ambao wamezaliwa Jumatano (July 24) huko Jaipur, Rajasthan India.

Dr. S.D. Sharma, wa J.K. Lone Hospital amesema tatizo kama hilo ni nadra sana kutokea hususan kwa watoto wa kiume, na linafahamika kama ‘Dicephalic Parapagus’.Aliongeza kuwa tukio hilo ni la pili kutokea India.Daktari huyo aliendelea kusema kuwa mara nyingi watoto wenye ‘Dicephalic Parapagus’ huzaliwa wakiwa wamekufa, na mara nyingi hutokea kwa watoto wa kike. Kwa mujibu wa Sharma alisema kuna uwezekano wa kuokoa maisha ya mapacha hao.

Rital na Ritag Gaboura wa Sudan baada ya kutenganishwa Inasemekana tatizo la mapacha kuzaliwa wameungana hutokea mara moja kati ya watoto 100,000 wanaozaliwa.
0 comments:
Post a Comment